1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

10 wauwawa Saudi Arabia

18 Novemba 2007

RIYADH:

Watu 10 wameuwawa pale moto uliporipuka katika bomba la gesi karibu na kinu cha gesi cha Hawiyah, nchini saudi Arabia jana usiku.

ARAMCO-kiwanda cha serikali cha mafuta na gesi kimesema katika taarifa yake kuwa moto huo ulisababishwa na kuvuja kwa gesi katika bomba liliopo km 30 kutoka kiwanda hicho.Moto huo sasa umedhibitiwa.

Haikufahamika haraka watu wa ngapi wamejeruhiwa pamoja na uraia wa waliofikwa na maafa hayo.

Kiwanda cha gesi cha Hawiyah kinazalisha mapipa 310.000 ifikapo 2008.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW