138 WAMEFARIKI KATIKA AJALI YA NDEGE:
1 Januari 2004Matangazo
COTONOU: Si chini ya watu 138 wamefariki katika ajali ya ndege iliotokea wiki iliopita katika pwani ya Benin-Afrika ya Magharibi.Kwa wa mujibu wa maafisa nchini Benin,watu wengine 2 bado hawajapatikana.Abiria 21 waliweza kuokolewa wakiwa hai.Inadhaniwa kuwa sababu ya ajali hiyo ni kuwa ndege ilibeba mizigo kuliko vile inavyoruhusiwa.Ndege hiyo ya shirika la Kilibnani UTA baada ya kuondoka uwanja wa ndege wa Cotonou iligonga jengo na baadae ikaangukia baharini.
