1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIndia

15 wafariki baada ya kunaswa na umeme, India.

20 Julai 2023

Watu 15 wamekufa nchini India baada ya kunaswa na umeme walipokuwa wakiandamana kupinga mradi wa serikali wa kuanzisha bwawa, ambao awali ulisababisha pia kifo cha mtu mmoja katika mazingira kama hayo.

Indien I 75. Jahresfeier Unabhängigkeit
Picha: Dasarath Deka/ZUMA/picture alliance

Maafisa wanne wa usalama ni miongoni mwa watu waliofariki kwenye tukio hilo.

Watu wengine 11 wamejeruhiwa katika ajali hiyo ya umeme iliyotokea katika wilaya ya Chamoli katika jimbo la kaskazini la Uttarakhand. Afisa mkuu wa wilaya ya Chamoli, Himanshu Khurana, amesema hapo jana kwamba uchunguzi unaendelea kubaini chanzo cha ajali hiyo.

India imekumbwa na mvua kubwa katika siku chache zilizopita, huku watu wengi wakipoteza maisha kutokana na mafuriko na maporomoko ya ardhi.

Jana usiku, watu watano wameripotiwa kufariki na wengine wamekwama chini ya vifusi katika Jimbo la magharibi la Maharashtra kufuatia maporomoko ya udongo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW