16 watiwa nguvuni kwa shutuma za ugaidi Uhispania
15 Juni 2005Matangazo
Madrid:
Polisi nchini Uhispania wamewatia nguvuni watu 16 wanaoshukiwa kuwa wanaharakati wa Kiislamu wa msimamo mkali . 11 kati yao wanadaiwa kuwa na mafungamano na Kiongozi wa al Qaeda nchini Iraq Abu Musab al-Zarqawi. Wengine watano wanashukiwa kuhusika na kuripuliwa treni ya abiria mjini Madrid mwezi Machi mwaka jana. Maafisa wa sheria wanasema watu hao walikamtwa mjini Barcelona ikiwa ni sehemu ya operesheni za pamoja za majaji wawili wanaoongoza uchunguzi tafauti. Uhispania imeshawatia nguvuni jumla ya watuhumiwa 200 , wanaharakati wa Kiislamu wa msimamo mkali. Kesi dhidi ya watuhumiwa 24 wa kundi la al- Qaeda inaendelea mjini Madrid.