1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

19. Agosti, siku ya misaada ya kiutu

19 Agosti 2020

Nchini jamhuri ya kidemokrasia ya Congo maelfu ya wakimbizi na wahamiaji katika mkoa wa kivu kusini wanalalamika kutokana na maisha magumu wanayopitia, huku mashirika ya kiutu yakielezea hali ngumu ya ukosefu wa usalama.

Kongo | Flüchtlinge in Ituri
Picha: imago-images/Xinhua/A. Uyakani

Wakiwa wanaishi ndani ya hema au ndani ya nyumba ndogo walizojenga kwa majani ya miti, baadhi ya wakimbizi katika mkoa wa kivu kusini wanashuhudia hali duni, wakihofia kuhusu hali ya afya ya jamaa zao na wameiomba serikali iwapatie msaada. Kwa kukosa na chakula, wakimbizi wengi wanalazimika kuomba-omba vijijini ijapokuwa vijiji vingi pia vimeporwa na wahalifu.

Kwa muda wa takribani miaka ishirini, vurugu za mara kwa mara kati ya makundi yanayo miliki silala zimesababisha maelfu ya watu kuyahama makaazi yao katika vijiji vingi vya mashariki ya jamhuri ya kidemokrasia ya Congo hususan katika mikoa ya Kivu ya kaskazini, kivu kusini, Ituri na Tanganyika. Hali hii imesababisha watu wengi kuyahama makaazi yao na kukimbilia misituni.

Mashirika ya kiutu yanafanyakazi katika mazingira magumu

Ujumbe wa udhibiti wa majanga wa Umoja wa UlayaPicha: picture-alliance/abaca/M. Thierry

Upande mwingine, baadhi ya mashirika ya kiutu yamelalamikia hali ya ukosefu wa usalama katika maeneo tofauti wanamo fanyia kazi ndani ya mkoa wa kivu kusini. Mnamo mwezi wa juni uliopita, mwanamke mmoja akiwa mtumishi wa shirika la MSF/Hollande alitekwa nyara na watu wenye silaha huko Fizi nakuachiliwa baada ya wiki tatu. Hali hii ilisababisha shirika hilo kufunga virago vyake huko Fizi hadi pale litakapo hakikishiwa usalama.

Soma zaidi: Wapiganaji Congo wadaiwa kuwauwa watu 1,300

Akizungumzia hali ya usalama katika wilaya ya Fizi, waziri wa mambo ya ndani katika mkoa wa Kivu Kusini, Lwabanji Lwasi Ngabo amekakumbushia nia ya viongozi kushughulikia wakaazi na pia kuwahakikishia usalama wao Aidha mafuriko ambayo yameripotiwa mjini Uvira mnamo miezi ya Machi na Aprili mwaka huu, pamoja na ajali za nyumba kuungua zilizo ripotiwa mjini Bukavu katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, zimeongeza pia idadi ya watu wanaohitaji misaada ya dharura kutoka serikalini bila kufanikiwa, wakati ambapo nadhari imeelekezwa kwenye mapambano dhidi ya janga la virusi vya corona.

Chanzo: DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW