1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

19 wauliwa na wanamgambo mashariki mwa Kongo

13 Machi 2023

Wanamgambo wanaoshukiwa kutoka katika kundi la uasi la ADF wamewaua watu wasiopungua 19 na kuchoma kituo cha afya katika kijiji cha Kirindera katika Jimbo la Kivu Kaskazini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Grenze DR Kongo Uganda Bunagana Flüchtlinge
Picha: Guerchom Ndebo/AFP/Getty Images

Mauaji yanaendelea kuripotiwa maeneo hayo licha ya juhudi za jeshi la Kongo, ambalo pia linapambana na kundi la waasi wa M23, ambalo mashambulizi yake katika miezi ya hivi karibuni yamepelekea watu 600,000 kuyahama makazi yao.

Hayo yanajiri wakati wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa walifanya ziara wikiendi hii huko Kivu Kaskazini.

Balozi wa Ufaransa katika Umoja wa Mataifa Nicolas de Rivière amesema Umoja wa Mataifa hauwezi pekee kupatia suluhu tatizo hilo, bali kunahitajika mazungumzo ya kisiasa na suluhisho la amani.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW