Jeshi la Ukraine latangaza mafanikio katika uwanja wa vita
8 Oktoba 2023Matangazo
Taarifa ya jeshi hilo imelitaja eneo la kusini mwa mji wa Bakhmut, karibu na kijiji cha Andriyivka, kuwa kumekuwa na mafanikio ya kiasi. Wakati mji huo ukiwa bado katika udhibiti wa Urusi, jeshi la Ukraine limefanikiwa kuidhibiti reli muhimu ya kimkakati.Katika uwanja wa mapambano kusini katika mkoa wa Zaporizhzhya, kuna kile Ukraine ilichokiita "mafanikio ya kiasi" yaliyopatikana kaskazini mwa vijiji vya Kopani na Novoprokopivka Kimsingi katika ukanda huo, jeshi la Ukraine limekuwa likikabiliana na ngome imara ya Urusi.