20 wauawa katika mripuko Mogadishu
3 Agosti 2008Matangazo
Mogadishu:
Mripuko wa bomu kandoni mwa barabara uliolilenga kundi la akina mama wafagiaji katika mtaa mmoja wa mji mkuu wa Somalia, umewauwa watu wapatao 20 na kuwajeruhi wengine kadhaa.
Mripuko huo ulitokea wakati kundi la akina mama wakisaidiwa na mashirika yasiokua ya kiserikali walipokusanyika kuufagia mtaa mmoja uliojaa taka. Mripuko huo ni mbaya kuwahi kushuhudiwa dhidi ya raia mjini Mogadishu kwa wiki kadhaa. mashahidi wanasema huenda idadi ya majeruhi ikaongezeka.