1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

2020: Miaka 60 tangu kuzinduliwa vidonge vya kuzuia ujauzito

Zainab Aziz Mhariri: Iddi Ssessanga
19 Agosti 2020

Vidonge hivyo vilishangiliwa na pia kulaaniwa vilikuwa ni mkombozi aliowapa wanawake fursa ya kujiamulia. Vilipoanzishwa viliigawa jamii. Kwa sasa umuhimu wake unazidi kunapungua.

Anti-Baby-Pille
Picha: picture-alliance/PYMCA/Photoshot

Leo tarehe 19.08.2020 imetimia miaka 60 tangu kuanza kutumika kwa vidonge vya kuzuia ujauzito vilivyoanza kutumika huko nchini Marekani mnamo mwaka 1960 na mwaka mmoja baadae vidonge hivyo vilianza kutumika nchini Ujerumani. Kwa mara ya kwanza akina mama walipewa uwezo wa kuamua juu ya miili yao. 

Kampuni za madawa ziliuza vidonge hivyo kama njia ya kuzuia maumivu ya hedhi. Hata hivyo wakati huo madaktari waliruhusu dawa hizo kwa ajili ya wanawake walioolewa tu.Lakini maandishi madogo yaliyojificha kwenye vipaketi vya dawa hizo yalisema vidonge hivyo pia vinazuia ujauzito. Vidonge hivyo viliaminika na viliwapa wanawake uwezo wa kufanya maaumuzi juu ya miili yao na kimsingi maisha yao yalibadilika.

Mwanaharakati wa kutetea haki za wanawake na mchapishaji bi Alice Schwarzer amesema wakati huo suala muhimu lilihusu kuzuia mimba ambazo hazikupangwa. Maisha ya wanawake wakati huo yalielekezwa katika kutambua kwamba haikuwezekana kutoa ujauzito, ilikuwa hatua ya kusisimua baada ya vidonge hivyo kuanza kutumika n chini Ujerumani, wanawake wote walifurahia hatua hiyo.Katika upande mwingine masuala matatu yalikuwa ya kipaumbele, yaani watoto, kazi za jikoni na dini. Tahadhari zilitolewa na madaktari juu ya dawa hizo na baba mtakatifu alizipiga marufuku.

Mwanaharakati wa kutetea haki za wanawake na mchapishaji Alice SchwarzerPicha: picture-alliance/dpa/R. Scheidemann

Kutokana na jamii kuwa ya kihafidhina nchini Ujerumani suala la uhuru wa akina mama kuamua juu ya miili yao halikuwamo katika ajenda baada ya kumalizika vita vikuu.Msimamo mkali wa kupinga matumizi ya dawa hizo za kuzuia uzazi ulitoka kwenye kanisa.Tarehe 25 mwezi Juni mwaka 1968 baba mtakatifu Paul wa 6 alilaani matumizi ya vidonge hiyvo. Alisema matumizi ya vidonge hiyvo yalichochea zinaa na tabia ya kwenda kinyume na maadili.

Tamko la kiongozi huyo wa  kanisa katoliki duniani lilikuwa na maana ya kuwapiga marufuku wakatoliki wote kutumia vidonge hivyo. Hata hivyo enzi hizo zilikuwa za usasa. Nguzo za Mfumo wa kijamii wa kizamani zililikuwa tayari zinayumba. Hali nzuri ya maisha iliyokuwa inaimarika ilihimiza uhuru wa kila mtu kuyatimiza malengo yake mwenyewe.

Mapinduzi ya mapenzi yaliondoa hulka za kihafidhina.Vija waliojulikana kama vijana  wa  furaha Hippies walifuata  kaulimbiu iliyosema" badala  ya vita tufanye mapenzi. Vijana hao walisema mwiko kutembea na mtu mmoja mara mbili la sivyo atakuwamo katika tabaka la watawala.

Hata hivyo wataalamu walijibu kwa kueleza kwamba matumizi ya vidonge vya kuzuia ujauzito hayakuwa chanzo cha harakati za vijana hao bali ilikua chachu tu. Wasichana na wanawake walioelewa sasa walikuwa na uhuru wa kuamua juu ya miili yao.  Hata hivyo stahamala imeongezeka juu ya matumizi  ya vidonge vya kuzuia ujauzito. Akina mama hawako tayari kufanya yale yanayoweza kutibua michakato asilia ya homoni.

Mtaalamu wa magonjwa ya wanawake Gabriella Stöcker amesema, wakati vidonge hivyo ni njia nzuri ya kujikinga, pia ni dawa yenye madhara yasiyotarajiwa.Daktari huyo ametahadharisha juu ya hatari ya  makampuni kugeuza dawa hizo kuwa mtindo wa  maisha. Ameeleza kwamba vidonge hivyo vinaweza  kumfanya mtu awe na umbo jembamba la mwili na kufanya ngozi ya mtu iwe nyororo, makampuni hayo yanaficha madhara yanayoweza kutokea kwa akina mama. Kwa mfano matumizi ya dawa hizo kama mtindo  wa maisha yanaweza kusababisha uvimbe unaoweza kusababisha msongamano wa damu – Thrombosis.

Mtaalamu wa historia ya utatibu Robert Jütte alipozungumza na DW alikumbuka maudhui ya tamko la Ulmer la mwaka 1964. Madaktari walitahadharisha juu ya kutokea madhara makubwa kutokana na mapenzi yasiyozaa matunda. Tahadhari hiyo ilitolewa na madaktari wapatao 200. Mtaalamu huyo anakumbuka juu ya kampeni iliyokuwa na lengo la kuzuia matumizi ya vidonge hivyo vya kuavya ujauzito.

Chanzo:/DW

 

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW