4,000 ndio wamarekani waliokufa Iraq
24 Machi 2008Wakati idadi ya wanajeshi wa Marekani waliopoteza maisha yao katika mgogoro uliodumu miaka mitano nchini Iraq ikiwa imegonga elf 4,hata hivyo idadi ya wanajeshi wa Iraq ni mara tatu zaidi ya hapo.Wao raia wa kawaida ambao wamekufa kutokana na mgogoro huo wanazidi 10,000.
Mgogoro wa Iraq ambao sasa umeingia mwaka wake wa sita umesababisha vifo vya wanajeshi wa Marekani wanofikia 4,000.Idadi hiyo imefika baada ya wanajeshi wengine wanne kuuliwa mjini Baghdad wakiwa wanashika doria.
Lakini idadi jumla ya wanajeshi ambao si wamarekani pamoja na raia wa kawaida ni kubwa mno kuliko ya wanajeshi wa Marekani.
Kuna habari za kutatanisha kuhusu idadi kamili sio tu ya wanajeshi wa Iraq ambao wameuawa katika mzozo huo lakini pia na raia wa kawaida.
Shirika moja la kigeni linalochunguza wahanga wa Iraq linaripoti kuwa wanajeshi wa Iraq ambao wamekufa tangu Marekani kuvamia nchi hiyo mwaka wa 2003 wanafikia elf8.Lakini serikali ya Baghdad, mwaka jana, ilitoa idadi yake ikionyesha kuwa wanafikia 12,000.Tena idadi ya raia wa kawaida waliopoteza maisha yao katika mgogoro huo mmoja inakadiriwa kuwa10,000 au zaidi.
Shirika linalofuatilia majeruhi nchini Iraq la icasualties.org, likitumia ripoti ambazo zinachapishwa na vyombo vya habari,kupitia wavuti wake linaonyesha kuwa wanajeshi wa Iraq wamekufa wengi kuliko wa Marekani na kuwa raia wa kawaida ,wao idadi yao kamili ni vigumu kujulikana, kwani vifo vya wengi havitangazwi na vyombo vya habari.
Mwezi januari uchunguzi wa pamoja kati ya serikali ya Iraq na shirika la Umoja wa Mataifa la afya,WHO,ulionyesha kama raia wa iraq kati ya 104,000 na 223,000 wameuawa tangu uvamizi uanze.
Machi 24,wavuti wa kujitegemea unaohesabu vifo vya raia wa Iraq,ukiegemeza matokeo yake na taarifa ambazo zinatolewa na vyombo vya habari uligusia idadi ya raia waliokufa kuwa 90,000 ukiongeza kuwa zaidi ya robo yao ambayo ni 24,000 walikufa mwaka wa 2007.
Mwezi September mwaka jana,taasisi moja ya Uingereza,ilikadiria idaid ya raia waliokufa kama zaidi ya millioni moja.Idadi hiyo inakwenda sambamba na ripoti iliotolewa hapo kabla na jarida la kiutibabu linaheshimika la Uingereza la Lancet.Ulipofika mwezi Julai mwaka wa 2006,uchunguzi uliotajwa na jarida la Lancet, uligundua kuwa takriban raia 655,000 zaidi walikufa kinyume na ikiwa kusingetokea vita.
Miongoni mwa raia waliokufa ni wale waliouawa kimakosa katika mashambulio ya ndege za majeshi ya ushirika unaoongozwa na marekani wakati yakilenga wapiganaji wa chini kwa chini.
Ingawa hakuna idadi kamili,lakini kwa mujibu wa Umoja wa mataifa raia 123 pekee waliripotiwa kuawa na hujuma za ndege katika kipindi cha miezi sita kati ya Julai mosi mwaka wa 2007 na disemba 31 mwaka huohuo mmoja.
Kulingana na icasualties.org,wanajeshi 308 kutoka nchi zingine wameuawa.Na vifo vya wanajeshi miongoni mwa nchi ambazo baado zinaaskari wao huko hadi ilipofikia 24 Mach ni kama ifuatavyo:Uingereza 175;Poland:23;Ukraine:18; Bulgaria:13; Na Denmark:8.
Kwa nchi ambazo mwanzo zilishiriki huko na baadae kuondoa majeshi yake wanajeshi wao walliokufa Iraq ni Italy wanajeshi 33 na Uhispania 11.Idadi ya waliofariki haiwahusu mamluki kadhaa ambao Marekani inawaita Makontarakata wa ulinzi.Idadi ya vifo vyao mwaka jana ilikadiriwa kuwa kati ya 140 na 900.
Na waandishi habari nao wamekumbwa na mgogoro huo ambao kwa mujibu wa shirika linalochunguza uhuru wa wanahabari,JFO,wandishi wa habari wa Iraq na wa kigeni waliokufa nchini Iraq tangu mwaka wa 2003 wamefikia 233.