47 WAUWAWA MOSUL
11 Machi 2005Matangazo
MOSUL:
Si chini ya watu 47 wameuwawa katika hujuma ya mtu aliejitoa mhanga katika mji wa Mosul, kaskazini mwa Iraq.Hii ni kwa muujibu wa taarifa za wakuu katika hospitali 2 kuu ambako watu hao walipelekwa.Kiasi cha watu wengine 100 wamejeruhiwa .Hujuma hii imetokea wakati waombolezi walipokusanyika katika ukumbi mmoja karibu na msikiti kwa mazishi ya waumini wa madhehebu ya shiia.