1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

71 wauwawa Somalia

21 Aprili 2007

HABARI KAMILI:

MOGADISHU:

Mashambulio ya mizinga katika mji mkuu wa Somalia-Mogadishu yameua hadi leo wasomali 73 huku mamia yakiuhama mji mkuu huo.

Jeshi la Ethiopia linaloisaidia serikali ya mpito ya Somalia imefyatua mizinga na makombora kutoka qasri la rais kusini mwa Mogadishu upande wa vituo kadhaa vya waasi wa kiislamu.Hii ikasababisha jibu kali la hujuma za waasi hao.

Hapo alhamisi Umoja wa Mataifa ulionya kuzuka msiba mkubwa wa wanadamu nchini Somalia huku maiti zikiozeana majiani mjini Mogadishu.Usiku mzima mapigano yakiendelea .

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW