1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroMamlaka ya Palestina

Abbas asema ataitembelea Gaza, licha ya kitisho cha usalama

15 Agosti 2024

Zaidi ya Wapalestina 40,000 wameuwawa katika vita vya Israel dhidi ya Hamas huko Gaza. Haya ni kwa mujibu wa wizara ya afya ya Palestina inayoendeshwa na kundi la Hamas.

Mahmoud Abbas aahidi kuutembelea ukanda wa Gaza
Mahmoud Abbas aahidi kuutembelea ukanda wa GazaPicha: Jordan TV/REUTERS

Haya yanafanyika wakati ambapo duru mpya ya mazungumzo ya kusitisha mapigano ikiwa imeanza huko Doha Qatar, kwa mujibu wa afisa mmoja aliyezungumza na shirika la habari la Reuters.

Mkutano huo wa faragha unahudhuriwa na maafisa wa Israel, Marekani, Misri na waziri mkuu wa Qatar. Marekani inatarajia kwamba makubaliano ya kusitisha vita yatafikiwa ili kuepusha Iran kufanya mashambulizi ya kulipiza kisasi wakati ambapo Marekani yenyewe, imeshapeleka manowari na ndege za kivita katika eneo hilo ili kuilinda Israel.

Wakati huo huo, Rais wa mamlaka ya Palestina Mahmud Abbas amekiambia kikao maalum cha jeshi la Uturuki leo kuwa atafunga safari na kuelekea Gaza, hata ikiwa safari hiyo itagharimu maisha yake.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW