1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Abbas, Haniye wakubaliana kuunda kamati ya maridhiano

31 Julai 2023

Viongozi hasimu wa kisiasa wa Kipalestina wanaokutana nchini Misri walisema kwamba pande hizo mbili zingeliunda kamati ya pamoja ya kujenga maridhiano ya ndani ya Palestina

Ägypten Versöhungsgespräche mit der Hamas
Picha: Thaer Ganaim/apaimages/IMAGO

Rais Mahmud Abbas na kiongozi wa kundi la Hamas, Ismail Haniyeh, walikutana kwa mazungumzo ya nadra ya ana kwa ana katika mji wa pwani wa El-Alamein pamoja na wawakilishi kutoka makundi ya kisiasa ya Kipalestina.

Jaribio hilo la karibuni kabisa la maridhiano linalenga kuziunganisha serikali mbili zinazoendeshwa sambamba za Hamas katika Ukanda wa Gaza uliozingirwa Israel na ile ya Mamlaka ya Palestina -- inayodhibitiwa na vuguvu la Fatah lake Abbas -- ambalo linatawala katika maeneo yanayoendeshwa na Palestina ya Ukingo wa Magharibi.

Soma zaidi: Pande pinzani nchini Palestina zaandaa mkutano wa pamoja kuhusu Israeli na UAE

Hamas na Fatah wafikia mwafaka wa mshikamano

Abbas na Haniyeh waliungana na wakuu wa makundi mengine, isipokuwa wa kundi lenye nguvu la Islamic Jihad na makundi mengine mawili madogo.

Haniyeh alisema bunge jipya, litakalojumuisha pande zote lazima liundwe kwa msingi wa uchaguzi wa kidemokrasia.

Naye Abbas akasema lazima pande zote zirudi kwenye dola moja, mfumo mmoja, sheria moja na jeshi moja halali.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW