1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Abbas: Mzozo wa Gaza ni zaidi ya kuangamiza wapalestina

27 Desemba 2023

Kiongozi wa mamlaka ya Palestina Mahmoud Abbas ameyaelezea mashambulizi ya Israel yanayoendelea katika Ukanda wa Gaza kuwa zaidi ya vita vya maangamizi na kuilaumu Marekani kwa uendelezaji wa vita hivyo.

Kiongozi wa mamlaka ya Palestina Mahmoud Abbas
Kiongozi wa mamlaka ya Palestina Mahmoud Abbas Picha: Christophe Ena/AP/dpa/picture alliance

Abbas amesema watu wa Palestina hawajashuhudia vita kama hivi vya sasa, hata wakati wa janga la "Nakba" la mwaka 1948 lililoshudia kurufushwa kwa Wapalestina wengi katika ardhi yao na Israel. 

Soma pia:Mahmoud Abbas: Israel inaendesha vita vya maangamizi Gaza

Akizungumza na televisheni moja nchini Misri Abbas alisema kwa bahati mbaya kila wakati dunia, Baraza la Usalama na Hadhara kuu ya Umoja wa Mataifa wanapojaribu kukomesha vita hivyo, Marekani inatumia kura yake ya turufu na kukataa kusitisha mapigano. 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW