1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSudan

Abdel Fattah al-Burhan kukutana na Rais wa Misri mjini Cairo

5 Novemba 2024

Mkuu wa jeshi la Sudan Abdel Fattah al-Burhan aliwasili Cairo, Misri Jumatatu kukutana na Rais wa nchi hiyo Abdel Fattah al-Sisi, ikiwa ni ziara yake ya kwanza tangu Misri ikanushe kuhusika na mzozo unaoendelea Sudan.

Kiongozi wa jeshi la Sudan Abdel Fattah al-Burhan alipofanya ziara katika kambi ya jeshi la wanamaji ya Flamingo, Port Sudan mnamo Agosti 28,2023
Kiongozi wa jeshi la Sudan Abdel Fattah al-BurhanPicha: AFP

Msemaji wa ofisi ya rais Sisi, Ahmed Fahmy, ameliambia shirika la habari la Ufaransa AFP kwamba rais huyo atakutana na Burhan wakati wa ziara hiyo ya Cairo.

Burhan alialikwa na Sisi kwa Kongamano la 12 la Miji Duniani

Wakati huo huo, taarifa ya jeshi la Sudan imesema kuwa Rais Sisi alimualika Burhankwa Kongamano la 12 la Miji Duniani lililoandaliwa na Mpango wa Makazi ya Kibinadamu wa Umoja wa Mataifa (UN-Habitat).

Sudan hali ni mbaya na hakuna shara ya vita kumalizika

Ziara ya karibuni zaidi ya Burhan nchini Misri ilikuwa mwezi Februari alipokutana na Rais Sisi na kujadili maono ya serikali yake ya kumaliza vita na kuhakikisha amani na utulivu.

Watu 13 wadaiwa kuuawa na kundi la RSF

Misri na Sudan zina mpaka mrefu wa pamoja, na mwezi uliopita, Misri ilikanusha madai ya kiongozi wa kikosi cha wanamgambo chaRSF Hamdan Daglo kwamba jeshi lake limehusika katika mzozo nchini humo.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW