Tchiani apanga kuunda serikali ya mpito kwa miaka 3 Niger
20 Agosti 2023Matangazo
Akizungumza kupitia televisheni ya taifa Tchiani ameonya pia kuhusu mataifa ya nje kuingilia masuala ya ndani ya taifa hilo.
Kabla ya mpango wake huo, Tchiani amesema ataandaa mazungumzo ya kitaifa ndani ya siku 30 kulijadili hilo na Wa-Niger wote. Mazungumzo hayo yatatoa muelekeo wa kuundwa kwa katiba mpya.
Kiongozi wa mapinduzi Niger kuunda serikali ya mpito
Tangazo lake limejiri baada ya Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika Magharibi (ECOWAS) kusema kuwa viongozi wake wa ulinzi wanapanga kuuingilia mzozo huo iwapo uongozi unaozingatia katiba hautarejeshwa nchini humo.
Jenerali Tchiani aliingia madarakani mwezi uliopita baada ya mapinduziwakati walinzi wa rais walipomkamata rais Mohammed Bazoum na kuchukua madaraka.