1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ABIDJAN : Ratiba ya kusalimisha silaha bado kupangwa

8 Mei 2005

Maafisa wa jeshi na viongozi wa waasi nchini Ivory Coast wamemaliza mazungumzo ya siku tano bila ya kupanga tarehe ya kuanza kusalimisha silaha kama ilivyokubalika katika makubaliano ya amani ya mwezi uliopita.

Mkutano huo ni sehemu ya makubaliano hayo yaliosainiwa nchini Afrika Kusini kwa lengo la kukomesha vita vya wenyewe kwa wenyewe katika nchi hiyo iliyogawika ya Afrika ya Magharibi na kuweka misingi ya kufanyika kwa uchaguzi huru hapo mwezi wa Oktoba.

Alain Richard Donwahi ambaye aliongoza kamati ya upatanishi ameweka matumani kwenye mazungumzo hayo kwa kusema kwamba ratiba ya kusalimisha silaha itawasilishwa kwa wakuu wa kijeshi kutoka pande zote mbili hapo Ijumaa ijayo ili iweze kuidhinishwa.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW