1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ABIDJAN: Serikali na waasi kupokonyana silaha

25 Desemba 2003
Majeshi ya serikali ya Ivory Coast na waasi wa zamani wanazazamiwa kukamilisha leo zoezi la kukusanya silaha zao na kuondoa mlolongo wa vizuwizi vilivyotawanywa barabarani katika muda wa mwaka na nusu wa mzozo wa kisiasa na kijeshi katika nchi hiyo ya Afrika magharibi. Kwa mujibu wa msemaji wa jeshi la serikali. Luteni Kanali Aka N'Goran, kila upande ulitakiwa kuwa umetekeleza leo maagizo waliyokubaliana hapo Disemba 10 wakati wa kikao cha viongozi wakuu wa jeshi la serikali na waasi uliyofanyika katika mji mkuu wa pili wa Bouaké unaodhibitiwa na majeshi ya waasi wa kaskazini mwa Côte d'Ivoire.
Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW