ABIDJAN: Walinzi wa amani wa Morocco wasitishwa kazi
22 Julai 2007Matangazo
Kikosi cha wanajeshi 800 wa Morocco kilicho sehemu ya majeshi ya Umoja wa Mataifa kulinda amani nchini Ivory Coast kimeachishwa kazi kwa muda,kwa sababu ya madai kuwa walihusika na dhuluma za ngono pamoja na watoto.Kikosi hicho, katika mji wa Bouake,kaskazini mwa nchi kimeamriwa kubakia kambini na kimesimamishwa kazi kwa hivi sasa.Wanajeshi wanaotumikia tume ya Umoja wa Mataifa hawaruhusiwi kuwa na uhusiano wa kijinsia na wenyeji.Mara kwa mara lawama za dhuluma za ngono zimetolewa dhidi ya walinzi wa amani wa Umoja wa Mataifa,sehemu mbali mbali za dunia.Kufuatia lawama hizo,Katibu Mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa,Kofi Annan alitanagaza kuwa vitendo vya aina hiyo havitostahmiliwa kabisa na Umoja wa Mataifa.