ABIDJAN:Prodi kuzuru Afrika Magharibi
11 Novemba 2003Matangazo
Rais wa Tume ya Umoja wa Ulaya Romano Prodi leo anatazamiwa kuanza ziara ya siku tatu ya Afrika Magharibi mjini Dakar Senegal ambayo pia itamfikisha Ivory Coast na Burkina Faso.
Kwa mujibu wa taarifa iliyopokelewa na shirika la habari la AFP mjini Dakar wiki iliyopita Prodi atakutana na Rais wa Senegal Abdoulaye Wade leo hii kuyakinisha mazungumzo kati ya Afrika na Umoja wa Ulaya kabla ya kuzuru kisiwa cha Goree ambayo ilikuwa bandari mashuhuri ya kusafirisha watumwa duniani kwa takriban karne nne.
Baadae Prodi atakwenda Ivory Coast ambapo atakuwa na mkutano wa siku moja na maafisa waandamizi wa nchi hiyo akiwemo Rais Laurent Gbagbo na waziri mkuu Seydou Diarra kujadili mnyakato wa amani unaosambaratika katika nchi hiyo iliogawika.
Prodi atakamilisha ziara yake ya Afrika Magharibi kwa kuitembelea Burkina Faso.