1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ABIDJAN:Wanajeshi wa Ufaransa kuchunguza mauaji

7 Januari 2004
Wanajeshi wa kulinda amani wa Ufaransa leo hii wamekuwa wakichunguza mauaji ya wafanyakazi sita wa kigeni wa Afrika Magharibi wakiwemo watoto watatu waliokatwa kwa mapanga hadi kufa katika kile kinachoonekana kuwa shambulio la karibuni kabisa dhidi ya wageni katika nchi hiyo ya Ivory Coast iliobarikiwa na zao la kakao. Shambulio hilo limetokea hapo Jumatatu karibu na Bangolo mji ulioko katika eneo lililositishwa mapigano la magharibi ambapo wanajeshi wa Ufaransa wanapiga doria.Mji huo uko kama kilomita 500 kutoka mji mkuu wa kibishara wa Ivory Coast Abidjan.
Kwa mujibu wa mashahidi wa mauaji hayo watu wasiojulikana wakiwa na bunduki na mapanga waliwashambulia wafanyakazi hao katika kijiji cha Kahin.