1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wafanyakazi wa treni na viwanja vya ndege wagoma Ujerumani

Sylvia Mwehozi
7 Machi 2024

Ujerumani imekabiliwa na migomo kwa miezi kadhaa sasa, huku wafanyakazi na uongozi wakishindana juu ya madai ya nyongeza ya mishahara, katikati mwa mfumuko mkubwa wa bei na kuyumba kwa biashara.

Treni za Ujerumani Frankfurt
Treni za masafa marefu za UjerumaniPicha: Thomas Lohnes/Getty Images

Wafanyakazi wa reli na viwanja vya ndege nchini Ujerumani, wameanza mgomo mkubwa leo kushinikiza nyongeza ya mishahara. 

Ujerumani imekabiliwa na migomo kwa miezi kadhaa sasa, huku wafanyakazi na uongozi wakishindana juu ya madai hayo, katikati mwa mfumuko mkubwa wa bei na kuyumba kwa biashara.

Wafanyakazi wa reli walianza mgomo wa masaa 35 katika treni za mizigo tangu jana Jumatano, huku mgomo wa treni za abiria ukianza leo asubuhi. Chama cha madereva wa treni cha GDL kinashinikiza kupunguzwa masaa ya kazi kwa wiki kutoka masaa 38 hadi 35.

Shirika la reli la Deutsche Bahn limelaani mgomo huo, likisema limefanya makubaliano ya nyongeza ya asilimia 13 ya mishahara. Wakati huo huo, wafanyakazi wa shirika la ndege la Ujerumani Lufthansa, nao watafanya mgomo wa nchi nzima kuanzia leo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW