1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiUfaransa

Abiria walioshukiwa kusafirishwa kinyemela warejeshwa India

26 Desemba 2023

Ndege moja ya kukodi iliyozuiwa kwa siku kadhaa nchini Ufaransa kufuatia mashaka kwamba abiria wake walikuwa sehemu ya mpango wa biashara haramu ya kusafirisha watu imetua mjini Mumbai nchini India usiku wa kuamkia leo.

Uwanja wa Ndege wa Vatry, mashariki mwa Ufaransa.
Ndege iliyozuiwa Ufaransa baada ya mashaka ya kusafirisha watu kinyemela kuwapeleka Nicaragua.Picha: Christophe Ena/AP Photo/picture alliance

Karibu abiria wote 300 waliokuwemo ndani ya ndege hiyo aina ya Airbus chapa 340  walikuwa na asili ya kihindi na walikuwa njiani kwenda nchini Nicaragua.

Safari yao ilianzia huko Umoja wa Falme za Kiarabu lakini ndege yao ilizuiwa kuondoka pale ilipotua kwa muda kwenye uwanja wa ndege wa Vatry, mashariki mwa Ufaransa, alhamisi iliyopita.

Mamlaka zilidokezwa kwamba abiria waliokuwepo huenda waliokuwa wanasafirishwa kwenda kutumikishwa huko Amerika ya Kusini.

Baada ya siku kadhaa za uchunguzi, abiria 276 kati ya 303 walikuwemo wamerudishwa India kwa kutumia ndege hiyo na wengine waliosalia watapatiwa hifadhi nchini Ufaransa.

Ruka sehemu inayofuata Gundua zaidi