1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Abiria Nigeria kusafiri kwa nusu nauli katika kipindi hiki

22 Desemba 2023

Rais wa Nigeria Rais Bola Tinubu ametangaza punguzo la nusu nauli katika msimu huu wa likizo kwenye vyombo kadhaa vya usafiri wa umma.

Nigeria gewinnt den Antrag auf Aufhebung des Schadensersatzes in Höhe von 11 Milliarden US-Dollar für den gescheiterten Gasvertrag
Picha: Temilade Adelaja/REUTERS

Rais Tinubu pia amesema usafiri wa treni utakuwa bure kuanzia jana Alhamisi, hatua inayolenga kuwarahisishia watu angalau kwa muda hali ngumu ya kiuchumi inayosababishwa na mpango wake wa kubana matumizi ya serikali.Athari za hatua hizo za kubana matumizi ya serikali zimeongeza gharama ya maisha kwa mamilioni ya watu ambayo tayari wanakabiliwa na athari za mfumuko wa bei. Nigeria, taifa lenye zaidi ya watu milioni 210 na lenye uchumi mkubwa zaidi barani Afrika lakini watu wake wanakabiliwa na umaskini mkubwa.Wanigeria mara nyingi huiona sikukuu ya Krismasi kama fursa ya mara moja kwa mwaka ya kuungana na familia katika maeneo ya vijijini, lakini mwaka huu ni watu wachache wanaosafiri huku raia wengi wakilazimika kuamua kati ya kusafiri au kuweka akiba ya fedha kwa ajili ya mahitaji ya msingi kama vile chakula.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW