SiasaEthiopia
Abiy Ahmed asema nchi yake haitoingia vitani na majirani
26 Oktoba 2023Matangazo
Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed amesisitiza leo kwamba nchi yake haitofuatilia maslahi yake "kupitia vita" baada ya matamshi yake ya awali ya kutaka nafasi ya kuitumia Bahari ya Shamu, kuzua hofu ya kikanda.
Akizungumza mbele ya maelfu ya wanajeshi wakati wa maadhimisho ya Siku ya Kitaifa ya Majeshi nchini Ethiopia, Abiy amesema Ethiopia haitoyatimiza malengo yake kupitia vita bali imedhamiria kufanya mazungumzo na majadiliano.
Mapema mwezi huu kupitia hotuba aliyoitoa kupitia televisheni, waziri mkuu huyo alisema Ethiopia ambayo haina bahari, ni nchi ambayo uhai wake unaitegemea Bahari ya Shamu na kwamba inataka bandari. Matamshi hayo yaliibua hofu hasa ukizingatia mivutano iliyoko baina ya Ethiopia na Eritrea.