ABUJA: Mgomo umekwamisha harakati za kiuchumi Nigeria
22 Juni 2007Matangazo
Vyama vya wafanyakazi nchini Nigeria,vimekula kiapo kuimarisha mgomo mkuu unaoendelea kwa siku tatu.Uamuzi huo ulipitishwa baada ya majadiliano kati ya Umoja wa vyama vya wafanyakazi na serikali kukwama jana usiku.Vyama vya wafanyakzi vinaitaka serikali iondoshe muongezeko wa bei ya mafuta iliyopandishwa kwa asilimia 20.Mgomo huo umekwamisha harakati nyingi za kiuchumi nchini Nigeria,huku shule,ofisi za serikali na vituo vya petroli vikiwa vimefungwa.Nigeria ni muuzaji mkuu wa nane wa petroli duniani.Hadi hivi sasa lakini, uchimbuaji na usafirishaji wa mafuta ya Nigeria haukuathirika.