ABUJA:Mateka waachiwa nchini Nigeria
17 Juni 2007Matangazo
Watu wenye siasa kali katika jimbo la mafuta kusini mwa Nigeria wamewaachia wahindi 10 waliowateka nyara wiki mbili zilizopita
karibu na bandari ya Harcourt. Watu hao ikiwa pamoja na jamaa wa familia zao walitekwa nyara kwenye makao yao.
Habari zaidi zinasema kuwa kuachiwa kwa mateka hao kunafuatia kuachiwa kwa dhamana, kwa kiongozi wa wanamgambo Dokubo Asari kutokana na sababu za kiafya.
Watu wenye siasa kali katika jimbo hilo la kusini mwa Nigeria wanapigania kuwa na usemi katika ugawaji wa mapato yanayotokana na utajiri wa mafuta.