ABUJA:mgomo mkuu kufanyika Nigeria leo
20 Juni 2007Matangazo
Vyama vya wafanyakazi vimekataa mapendekezo ya serikali ya Nigeria yenye lengo la kuepusha mgomo mkuu unaotarajiwa kuanza leo nchini humo.
Mwenyekiti wa chama kikuu cha wafanyakazi nchini Nigeria bwana Abdulwaheed Omar amesema ikiwa serikali inataka kuepusha mgomo huo, lazima ifute kabisa uamuzi wa kuongeza bei ya petroli badala ya kupunguza tu bei hizo.
Hatahivyo serikali ya Nigeria imekataa tashi hilo na badala yake imetoa mwito kwa wananchi juu ya kupuuza mgomo huo na waendelee na kazi zao kama kawaida.