ABUJA:Watu laki moja kupata madawa ya UKIMWI Nigeria.
25 Februari 2005Matangazo
Serikali ya Nigeria inakusudia kugawa dawa kwa watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI nchini humo, lakini hata hivyo inahofiwa kuwa watu wengi hawatanufaika na mradi huo.
Waziri wa afya wa nchi hiyo amesema kwamba watu laki moja watapatiwa dawa hizo katika mpango wa ruzuku iliyotengewa mwaka huu.
Nchini Nigeria kuna watu alfu14 tu wanaopata dawa hizo kwa bei ya dola saba kwa mwezi kwa kila mgonjwa.
Kwa mujibu wa takwimu Nigeria ina watu wapatao milioni tatu na nusu wanaougua ugonjwa wa UKIMWI.