1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ACT Wazalendo yazindua ilani yake ya Uchaguzi Mkuu

George Njogopa 22 Septemba 2025

Chama cha ACT Wazalendo Tanzania kimezindua rasmi ilani yake ya uchaguzi mkuu huku kikifanya mkutano wake mkubwa wa hadhara jijini Dar es salaam na kuwaleta pamoja viongozi wake wote.

ACT imeainisha vipaumbele saba vinavyomulika maeneo ya ukuzaji uchumi, maendeleo ya raia mmoja mmoja na miundombinu.
ACT Wazalendo yazindua ilani yake ya Uchaguzi MkuuPicha: Ericky Boniphace/DW

Chama hicho ambacho kimesimamisha wagombea wake wa ubunge kuanzia visiwani Zanzibar mpaka bara, kimeainisha vipaumbele saba vinavyomulika maeneo ya ukuzaji uchumi, maendeleo ya raia mmoja mmoja hadi katika maeneo ya miundombinu. Maneneo mengine ambayo chama hicho kimetamba kuyatekeleza kutokana na matumaini yake ya kupata wingi mkubwa wa idadi ya wabunge na madiwani ni pamoja na kujenga uchumi wa watu utakawezesha kuzalisha ajira zipatazo milioni 12.

Akianisha vipengele vya ilani hiyo mbele ya waandishi wa habari pamoja na baadhi ya wagombea wake, mmoja ya viongozi wa chama hicho, Emmanuel Mvula amesema katika utekelezaji ajenda ya ukuzaji uchumi chama hicho kimelenga kuanzisha masoko ya kimkakati yatayofanya kazi kwa saa 24.

Ama amesema masuala ya kusimamia haki na usalama wa raia, kulinda na kusimamia ardhi  pamoja na kuutetea muungano ni maeneo mengine ambayo yamezingatiwa katika ilani hiyo ambayo inazinduliwa katika wakati ambapo vumbi la kampeni likianza kuingia mwezi wa pili.

Chama hicho kimesema safu yake ya wagombea kuanzia ngazi za madiwani, ubunge na urais ndiyo watasukuma mbele ajenda ya ilani hiyo na kwa mujibu wa kiongozi wa chama hicho, Dorothy Temu wagombea hao ni wapambanaji walioiva. Viongozi mbalimbali wa chama hicho ikiwamo baadhi ya wagombea ubunge na udiwani walikuwa katika maeneo ya Segerea walikokata utepe wa kuinadi ilani hiyo.

Katibu Mkuu wa chama hicho, Ado Shaibu amesema licha ya kukabiliwa na mitihani mbalimbali wakati huu ikiwamo mgombea wake urais na mgombea mwenza kuenguliwa na mamlaka zinazosimamia uchaguzi huo, chama hicho bado hakijaondoka katika reli yake.

Wakati hayo yakiendelea, shauri lililetwa katika mahakama kuu kanda yaa Dodoma na mgombea urais wa ACT Wazalendo, Luhaga Mpina anayepinga kuenguliwa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi(INEC) limeanza kusikilizwa.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW