1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ADDIS ABABA: Balözi wa Israel nchini Ethiopia adaiwa kujipiga risasi

31 Machi 2005

Balozi wa Israel nchini Ethiopia Doron Grossman amepatikana akiwa amejeruhiwa vibaya katika chumba cha hoteli alikokuwa anakaa mjini Adis Ababa.

Baada ya kukisiwa kwamba huenda alivamiwa, wanadiplomasia na duru za afya wamenukuliwa wakisema balozi huyo alijaribu kujiuua mwenyewe. Balozi huyo amerejeshwa nchini Israel akiwa katika hali mahututi.

Kwa mujibu wa walinzi wa hoteli hiyo,walisikia mlio wa risasi na baadae walimkuta balozi huyo chini akiwa anavuja damu na bastola yake ikiwa kando.

Lakini duru za usalama za Israel zimesema tukio hilo linaonekana kusababishwa na masuala ya kibinafsi.Grossman mwenye umri wa miaka 48 ametumikia wadhifa huo tangu mwaka 2002 na alitarajiwa kuwa balozi wa Israel nchini Afrika Kusini.