1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ADDIS ABABA: Ethiopia itatetea serikali ya mpito ya Somalia

20 Julai 2006

Serikali ya Ethiopia imesema itailinda serikali ya mpito ya Somalia dhidi ya mashambulio yo yote yatakayofanywa na wafuasi wa Muungano wa Mahakama ya Kiislamu nchini Somalia(SICS).Waziri wa habari wa Ethiopia,Berhan Hailu amesema,wafuasi wa muungano huo wa Kiislamu,hawatoruhusiwa kuishambulia serikali ya rais Abdullahi Yusuf Ahmed mjini Baidoa,inayotambuliwa na jumuiya ya kimataifa.Mvutano kati ya serikali ya mpito ya Somalia iliyo dhaifu na Muungano wa mahakama ya kiislamu,umezidi tangu wanamgambo wa kiislamu kuudhibiti mji mkuu wa Somalia,Mogadishu mapema mwezi wa Juni na kuendelea kujiimarisha katika sehemu zingine za nchi.