1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ADDIS ABABA: Mafuriko yasababisha hasara ya maisha na mali

18 Agosti 2006

Mafuriko ya maji yameua hadi watu 900 kusini mwa Ethiopia na wengine kwa maelfu wamenasa juu ya mapaa ya nyumba na kwenye miti.Siku ya Alkhamisi wasaidizi waliwaokoa kama watu 6,000 katika eneo la kusini ambako Mto wa Omo ulifurika na kuua si chini ya watu 364.Serikali imeonya kuna hatari ya kutokea mafuriko kote nchini,baada ya mito mingine kufurika kaskazini,kusini,mashariki na magharibi mwa nchi.Vile vile mabawa makuu nchini humo yanakaribia kupasuka.Shirika la misaada la “Madaktari wasio na Mpaka” (MSF) limesema,zaidi ya watu 10,000 wamepoteza makazi yao katika mafuriko yaliyotokea karibu na ziwa la Tana kaskazini mwa nchi,lakini idadi hiyo huenda ikafikia 35,000 katika majuma yajayo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW