1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ADDIS ABABA : Mamilioni ya Waethiopia wapiga kura

15 Mei 2005

Mamlioni ya Waethiopia leo wamepiga kura katika uchaguzi wa bunge unaonekana kuwa mtihani muhimu wa demokrasia katika nchi hiyo ilioko kusini mwa Jangwa la Sahara barani Afrika nchi ya pili kwa kuwa na idadi kubwa ya watu barani humo.

Uchaguzi huo ambao ni wa pili wa vyama vingi katika nchi hiyo inayozalisha kahawa kwa wingi barani Afrika unatarajiwa kumpa ushindi wa kipindi cha tatu Waziri Mkuu Meles Zenawi ambaye amempinduwa dikteta Mengistu Haile Mariam hapo mwaka 1991 na kukomesha miaka 17 ya utawala wa Kimakrsisti.

Vyama vya upinzani vyenye kupigania kuwepo dhima kubwa kwa masoko huria katika nchi hiyo ya Pembe ya Afrika yenye watu milioni 72 vimeweka kando tafauti zao kwa mara ya kwanza na kuahidi kuungana iwapo itamaanisha kuwa na ushindi wa viti vingi katika bunge la taifa lenye viti 547.