Addis Ababa. Matokeo ya mwanzo ya uchaguzi, serikali yapata ushindi.
9 Julai 2005Matangazo
Matokeo ya mwanzo ya uchaguzi uliofanyika mwezi uliopita nchini Ethiopia yameipa serikali ushindi wa kiasi.
Tume ya uchaguzi ya taifa imesema kuwa matokeo rasmi kutoka zaidi ya nusu ya wilaya zilizofanya uchaguzi yamekipa chama tawala cha Ethiopian People’s Revolutionary Front pamoja na washika wake ushindi.
Matokeo hayo ni kama ya mwanzo ambayo yalisababisha ghasia zilizoambatana na umwagaji damu mwezi ulipita katika mji mkuu Addis Ababa.
Matokeo kamili hayatarajiwi hivi karibuni, yakingojea uchunguzi dhidi ya madai ya udanganyifu katika mjimbo zaidi ya 200 ya uchaguzi.
Vyama vya upinzani vimesema kuwa uchunguzi huo hauaminiki na wameitaka tume ya uchaguzi kurekebisha kasoro hizo.