1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ADDIS ABABA: Mauritania yashinikizwa kufuatia mapinduzi

5 Agosti 2005

Uanachama wa Mauretenia umeahirishwa na Umoja wa Afrika,baada ya maafisa wa kijeshi kumpindua rais Maaouya Ould Taya.Umoja huo wa madola 53 umeyalaani mapinduzi hayo na umedai kuwa utaratibu wa kikatiba urejeshwe.Umoja wa Mataifa,mkoloni wa zamani Ufaransa na Marekani pia zimelaani mapinduzi ya siku ya jumatano katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi.Kwa hivi sasa viongozi wa mapinduzi,wamemchagua mkuu wa zamani wa polisi,Ely Ould Mohamed Vall kuwa kiongozi mpya.Hali shuari iliyorejea kwa haraka katika mji mkuu yachukuliwa kama ni ishara kwamba wengi wameunga mkono mapinduzi ya kumuondosha rais Taya.