1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Addis Ababa. Uchaguzi nchini Ethiopia kufanyika Jumapili.

14 Mei 2005

Kiongozi wa Ethiopia amesema jana kuwa matukio ya hapa na pale ya ghasia kuelekea uchaguzi mkuu utakaofanyika kesho Jumapili hayataathiri upigaji wa kura wakati kampeni zinakamilika na huku rais wa zamani wa Marekani Bwana Jimmy Carter akitoa sifa tele.

Huku kukiwa na hali inayoendelea ya mkwamo katika kuteua siku ya kupiga kura kati ya chama tawala cha waziri mkuu Meles Zenawi na vyama vikuu viwili vya upinzani , wafadhali wa nchi hiyo masikini inayotegemea misaada wamezitaka pande zote kuepusha vitendo vya ghasia.

Bwana Meles ambaye anataka kuchaguliwa tena kwa kipindi cha tatu katika uchaguzi utakaofanyika Jumalipi alikubali kuwa kumekuwa na ukiukwaji wa utaratibu wa uchaguzi katika nchi hiyo , lakini aliliambia shirika la habari la AFP kuwa hali hiyo haiwezi kuharibu kile ilichokiita hatua za haki na uwazi za uchaguzi.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW