1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ADDIS ABABA: Vurugu za uchaguzi zazuka upya na watu kuuwawa

2 Novemba 2005

Malumbano baina ya polisi wa kuzima ghasia na waandamanaji mjini Addis Ababa yamesabisha milipuko ya bunduki na maguruneti huku polisi wakiwauwa takriban watu 33 katika vurugu zilizo zuka upya za kupinga matokeo ya uchaguzi nchini Ethiopia.

Mji wa Addis Ababa umekumbwa na milio mizito ya bunduki za rashasha kufikia hadi katika milango ya afisi za balozi za Uingereza, Ufaransa, Kenya na Ubelgiji zilizo sehemu tofauti mjini humo.

Wafanyakazi wa umoja wa mataifa wametakiwa kubaki ndani ya afisi zao.

Takriban watu 81 wamejeruhiwa pamoja na mtoto wa miaka saba ambae madaktari katika hospitali ya Black Lion wamesema amepigwa risasi ya pajani, na mwengine mwenye umri wa maika 13 ambaye amepata majeraha tumboni na miguuni katika vurugu hizo.