1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Addis Ababa. Vyama vya upinzani kususia bunge jipya.

10 Septemba 2005

Muungano wa vyama vya upinzani nchini Ethiopia unafikiria uwezekano wa kulisusia bunge jipya , wakisema kuwa sheria ambazo zilipitishwa katika dakika za mwisho la bunge la zamani zinalenga katika kuzuwia uwezo wao na kuwakera wabunge wa upinzani.

Sheria hizo mpya zinasema kuwa ni vyama vile tu ambavyo vina asilimia 51 ya wabunge , bungeni ndio vitakuwa na haki na kupendekeza hoja bungeni na kuleta ajenda zitakazojadiliwa katika bunge hilo, msemaji wa muungano wa vyama vya upinzani , Hailu Araya amesema leo.

Amesema kuwa sheria hizo zilikuwa na lengo la kuzuwia nguvu za vyama vya upinzani ambavyo vimepata jumla ya viti 174 katika bunge lenye viti 547 katika uchaguzi wa hapo May 15 mwaka huu , ikiwa ni mafanikio makubwa kutoka kuwa na viti 12 tu katika uchaguzi wa hapo mwaka 2000.

Hapo kabla vyama vilivyokuwa na asilimia 20 viliruhusiwa kupendekeza hoja bungeni.