1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ADDIS ABABA:Uingereza yafutilia mbali msaada wa ziada kwa Ethiopia

16 Juni 2005

Uingereza imefutilia mbali msaada wa ziada wa euro milioni 45 kwa nchi ya Ethiopia baada ya mauaji ya watu 36 katika maandamano dhidi ya matokeo ya uchaguzi.

Waziri wa maendeleo ya kimataifa nchini humo Hillary Benn ametangaza hatua hiyo alipozitembelea nchi za Afrika mashariki.

Benn alisema nchi yake iliitilia maanani sana hali mbaya iliyokuwa nchini humo.

Takriban watu 36 waliuwawa mjini Addis Ababa baada ya polisi kuwafyetulia risasi waandamanaji waliokuwa wakipinga udanganyifu wa kura.

Hapo jummne viongozi wa kisiasa nchini humo walitia saini makubaliano ya kujaribu kumaliza mzozo na kuanzishwa uchunguzi juu ya malalamoko ya kupitika udanganyifu katika uchaguzi wa Urais.

Kiongozi wa upinzani Haili Shawel aliyekuwa amewekwa kwenye kifungo cha ndani ya nyumba ameachiwa huru.