1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ADDIS ABABA:Vikosi vya Umoja wa Ulaya kubakia Darfur

21 Oktoba 2005

Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika-PSC limerefusha kwa miezi mitatu mamlaka ya vikosi vyake vya ulinzi katika eneo la Darfur,magharibi mwa Sudan ambako machafuko yanashika kasi.Uamuzi huo umepitishwa wakati ambapo wajumbe wa serikali ya Sudan na wa makundi mawili ya waasi wa Darfur wameahirisha majadiliano ya amani yanayosimamiwa na Umoja wa Afrika katika mji mkuu wa Nigeria Abuja.Wajumbe hao watarejea Abuja Novemba 20 na siku ya pili,majadiliano rasmi yataendelea.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW