1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Addisababa: Viongozi wa upinzani wanafuatwa na makachero huko Ethiopia

9 Juni 2005

Viongozi wa makundi makubwa ya upinzani huko Ethiopia wamesema bado wanachunguzwa sana na makachero wa serekali, lakini hawako tena chini ya vizuwizi vya nyumbani. Hii ni kufuatia mapambano makali baina ya polisi na waandamanaji yaliotokea mwanzoni mwa wiki. Maduka mengi katika mji mkuu wa Ethiopia yalibakia yamefungwa na maedereva wa taxui bado wako katika mgomo. Serekali imeonya kwamba michafuko mengine ya raia itashughulikiwa kwa ukali. Majeshi ya usalama ya Ethiopia yaliwafyetulia risasi waandamanaji katika mji mkuu wa Addisababa hapo jana na kuwauwa watu 22. waandamanaji wanadai kwamba kulifanyika udanganyifu mkubwa na vitisho katika uchaguzi wa bunge wa mwezi uliopita, na ambao serekali inadai imeshinda.