1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ADF yashukiwa kuwaua watu 10 mashariki mwa Kongo

13 Aprili 2024

Washambuliaji wanaoshukiwa kuwa waasi wa ADF wamewaua watu wasiopungua 10 karibu mji wa Beni mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Wanajeshi wa Kongo.
Jeshi la Kongo limekuwa likipambana dhidi ya uasi wa ADF na makundi mengine mashariki mwa Kongo kwa miaka mingi. Picha: Alain Uaykani/Xinhua/picture alliance

Taarifa hizo zimetolewa na mamlaka za eneo hilo na chanzo kimoja cha Umoja wa Mataifa.

Inaarifiwa washambuliaji waliwafyetulia risasi watu waliokuwa wakifanya kazi mashambani nje kidogo ya mji wa Beni. Hayo ni kwa mujibu wa meya wa mji mdogo wa Mulekera, Nongo Mayanga.

Amesema miili ya watu saba tayari imepatikana ikiwemo ya wanawake watatu na mingine mitano imebainika sehemu nyingine. Amesema wana wasiwasi kwamba miili zaidi ya watu itapatikana wanapoendelea na msako.

Kundi la ADF lilianzia Uganda lakini sasa linaendesha harakati zake mashariki mwa Kongo likiwa na mafungamano na kundi linalojiita Dola la Kiislamu. Wapiganaji wake hufanya mashambulizi ya kuvizia na kuongeza hali ya ukosefu wa usalama nchini Kongo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW