1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Adhabu ya kifo inakiuka haki za binadamu

20 Juni 2007

Wafungwa nchini Malawi wamepata afueni baada ya majaji watatu wa mahakama kuu kupitisha kwa kauli moja sheria ya kuzuia adhabu ya kifo kwa kuzingatia kuwa amri hiyo inakiuka haki za kibinadamu.

´Bendera ya Malawi
´Bendera ya Malawi

Uamuzi huo wa kihistoria nchini Malawi umewezesha kuondolewa kifungu cha sheria namba 210 ambacho awali kililisisitza kuwa adhabu ya kifo kwa kunyongwa ndio ilikuwa suluhisho kwa majaji waliosikiliza kesi za mauaji.

Adhabu ya kifo pia hutolewa kwa makosa ya jinai ubakaji na wizi wa kutumia nguvu nchini Malawi. Hatua hiyo muhimu imepongezwa na wanaharakati wanaopinga adhabu ya kifo.

Uamuzi wa majaji hao wa mahakama kuu pia unalenga maisha yanayowakabili wafungwa wakiwa gerezani na hata baada ya mahakama kuamua adhabu ya ania nyingine kwa mfano kifungo cha maisha.

Parvis Jabbar na Saul Lehrfreund mawakili wa haki za binadamu wa nchini Uingereza wamesema kwa sasa kesi za mauaji nchini Malawi zitachukua mueleko mpya na wameelezea furaha yao kwamba mfumo huo uliotumika nchini Uganda na katika maeneo mengine sasa umekubalika nchini Malawi.

Uamuzi huo wa majaji watatu wa mahakama kuu uliihushisha kesi ya Francis Kafantayeni na wenzake watano wanaokabiliwa na adhabu ya kifo katika jela ya Zomba nchini Malawi.

Kafantayeni alihukumiwa kunyongwa manamo mwaka 2002 baada ya kukiri kumuua mwanawe wa kambo wa miaka miwili, lakini alijitetea kuwa alitenda uhalifu huo kwa kuwa hakuwa na akili timamu.

Hukumu yake pamoja na hukumu za watu wengine watano zitasikilizwa upya mahakamani kuanzia mwishoni mwa mwezi huu.

Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu Amnesty International limesema kwamba hali mbaya katika jela za nchini Malawi inatishia maisha, katika ripoti yake ya mwaka huu shirika hilo limesema kuwa takriban vifo 280 vilitokea katika jela za nchi hiyo mwaka uliopita.

Kiwango cha vifo kimeongezeka kutoka vifo 14 kwa mwezi kwa mujibu wa orodha iliyoandikishwa mwaka 2005 shirika hilo limesema kuwa vifo vingi husababaishwa na ukosefu wa lishe bora.

Wafungwa wengi wana hali mbaya ya kiafya nchini Malawi na hali hii inahitaji kushughulikiwa kwa haraka.

Mawakili wa shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu wanawa wakilisha mahakamani bila malipo wafungwa wanaokabiliwa na adhabu kali katika nchi za Carrebean na Afrika.

Wanaharakati wanaopinga adhabu ya kifo wanataka adhabu hiyo ipigwe marufuku kabisa nchini Malawi.

Kwa kipindi cha miaka kumi iliyopita hata hivyo marais wawili hawakutia saini makaratasi ya kuwanyonga watu waliohukumiwa adhabu ya kifo.

Jaji Elton Singini amesema, adhabu ya kifo inakiuka haki za kibinadamu, awali agizo la adhabu ya kifo lilichangia pakubwa katika kumnyima mtu nafasi ya kuwakilishwa vyema mahakamani na pia kusikilizwa upya kesi yake katika mahakama ya juu.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW