1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

AFCON 2025 yazidi kupamba moto Morocco

25 Desemba 2025

Mechi za mzunguko wa kwanza katika kila kundi kwenye michuano ya AFCON 2025 inayoendelea nchini Morocco zimekamilika. Mabingwa watetezi wa kombe hilo Ivory Coast wameibuka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Msumbiji.

Morocco I 2025
Mashabiki wa kandanda nchini Morocco kwenye michuano ya AFCON 2025Picha: Abu Adem Muhammed/Anadolu/picture alliance

Mechi za mzunguko wa kwanza katika kila kundi kwenye michuano ya AFCON 2025 inayoendelea nchini Morocco zimekamilika.

Mabingwa watetezi wa kombe la mataifa barani Afrika AFCON, Ivory Coast wameanza safari yao kibabe baada ya kuibuka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Msumbiji.

Nyota wa Manchester UnitedAmad Diallo aliutia mpira wavuni mwanzoni mwa kipindi cha pili na kupeleka furaha kwa nchi yake. Mchezo huo mgumu ulichezwa mjini Marakesh huku kukiwa na mvua kubwa.

Katika mchezo wa mapema kabisa mjini Rabat, timu ya taifa ya Algeria ilimenyana na Sudan na kufanikiwa kuondoka na ushindi wa goli 3-0. Mchezaji wa zamani wa Manchester City Riyad Mahrez na mchezaji wa sasa wa Al-Ahliya Saudi Arabia aliibeba nchi yake kwa kuzisalimia nyavu za Sudan.

Nyota wa Misri, Mohammed Salah akishangilia goli lake katika mechi yao ya kwanza ya AFCON 2025- dhidi ya Zimbabwe.Picha: Franck Fife/AFP/Getty Images

Mahrez sasa ameweka rekodi ya kufikisha mabao nane katika michuano sita ya AFCONaliyocheza.

Zidane uwanjani.

Miongoni mwa watazamaji wa mechi hiyo ni gwiji wa UfaransaZinedine Zidane, ambaye wazazi wake walitoka Algeria na mtoto wake Luca alikuwa golini katika kikosi cha Mbweha wa Jangwani. 

Kuonekana kwake kwenye skrini kubwa uwanjani kuliibua shangwe kubwa kutoka kwa wafuasi wa Algeria ambao watakuwa wamefurahi kuona timu yao ikitoka na matokeo ya kuridhisha.

Kwingineko, bao la mapema la Karl Etta Eyong liliipaCameroon ushindi mnono wa 1-0 dhidi ya Gabon mjini Agadir na Burkina Faso wakafunga mabao mawili ndani ya muda wa nyongeza na kuilaza Equatorial Guinea 2-1 mjini Casablanca.

Wachezaji wa Chipolopolo Zambia katika mechi yao dhidi ya Mali.Picha: Sebastian Frej/SFSI/IMAGO

Ivory Coast, ambao wanamenyana na Cameroon na Gabon katika mechi zao zilizosalia za makundi, wanalenga kuwa taifa la kwanza tangu Misri mwaka 2010 kutetea kwa mafanikio taji la kwanza la soka barani Afrika.

Mechi za mzunguko wa pili zinatazamiwa kuanza tena hapo kesho. Misriwatacheza na Afrika ya Kusini mapema kabisa, Zambia watafuatia dhidi ya Comoro huku mechi ya usiku ikiwa ni kati ya wenyeji Morocco dhidi ya Mali. 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW