1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

AFCON: Matumaini ya Uganda kusonga mbele yafifia

28 Desemba 2025

Matumaini ya Uganda kufuzu kwa hatua ya mtoano ya Kombe la Mataifa ya Afrika yamefifia baada ya kutoka sare ya 1-1 dhidi ya Tanzania, katika mchezo uliochezwa Rabat.

AFCON
Tanzania itasaka ushindi wa kwanza katika michuano ya AFCONPicha: Wikus de Wet/AFP/Getty Images

Uganda ilipata nafasi ya kuibuka na ushindi dakika za mwisho, lakini Allan Okello alipoteza penalti muhimu.

Tanzania ilitangulia kupata bao kupitia penalti ya Simon Msuva dakika ya 59, kabla ya Uche Ikpeazu kusawazisha kwa kichwa dakika 10 kabla ya mechi  kumalizika. Sare hiyo inaiacha Uganda katika hali ngumu kwenye Kundi C, huku Tanzania ikisalia kutafuta ushindi wake wa kwanza katika michuano ya AFCON.

Nigeria inaongoza kundi C baada ya kuilaza Tunisia 3-2, Senegal ipo kileleni mwa kundi D pointi sawa na DRC baada ya kutoka sare ya 1-1.

Katika mechi nyengine za makundi Gabon itakuatana na Msumbiji, Guinea ya Ikweta itakipiga na Sudan. Algeria ikutane na Burkina Faso kisha Ivory Coast ipambane na Cameroon.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW