1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

AFCON yaikosesha usingizi Bayer Leverkusen

5 Desemba 2023

Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika zitakapoanza Januari, klabu katika ligi kuu ya Ujerumani Bundesliga zitakuwa bila ya wachezaji wao kadhaa muhimu.

Fußball Bundesliga Bayer 04 Leverkusen v 1. FC Köln | Jubel Victor Boniface
Mshambuliaji wa Bayer Leverkusen, Victor BonifacePicha: Marius Becker/dpa/picture alliance

Kutokuwepo kwao kwa wakati muhimu kunaweza kubadilisha jinsi vilabu vitakavyosajili wachezaji wa kandanda wa Kiafrika katika siku zijazo.

Mshambulizi wa Bayer Leverkusen, Victor Boniface anakumbuka kwa furaha wakati Nigeria iliposhinda taji lao la tatu na la mwisho la Kombe la Mataifa ya Afrika muongo mmoja uliopita. Anatazamiwa kucheza mchuano wake wa kwanza na Nigeria mwezi Januari,  na mshambuliaji huyo muhimu atakosekana katika klabu yake wakati akiichezea timu ya taifa.

Soma pia: Leverkusen haishikiki katika Bundesliga

"Ni ndoto ya kila mchezaji wa kandanda kutoka Nigeria kuwakilisha nchi yake na kushinda kombe kwa ajili ya nchi. Kwa hivyo tunatazamia AFCON ijayo," Boniface aliiambia DW baada ya kufunga bao lake la nane la Bundesliga katika sare ya 1-1 dhidi ya Borussia Dortmund katika uwanja wa BayArena huko Leverkusen.

Soma pia: Wenyeji wa AFCON Ivory Coast wapangwa kundi moja na Nigeria

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 ni mmoja wa wachezaji watano wa Leverkusen, akiwemo Odilon Kossounou, Edmond Tapsoba, Amine Adli na Nathan Tella, ambao wanaweza kuelekea kwa michuano ya AFCON 2023 nchini Ivory Coast mwezi Januari.

Michuano hiyo awali ilipangwa kufanyika Juni na Julai 2023, lakini ilisongezwa mbele kwa sababu ya hofu kwamba msimu wa mvua nchini Ivory Coast unaweza kutatiza ratiba ya mechi.

Kukosekana kwa Boniface, ambaye alichaguliwa kuwa Mchezaji mpya Bora wa Mwezi kwa miezi mitatu ya kwanza ya msimu wa Bundesliga, kutatatiza Leverkusen kwa kuwa kikosi cha kocha Xabi Alonso kinatazamia kushinda taji la Bundesliga kwa mara ya kwanza.

"Hatuna wasiwasi"

Edmond Tapsoba baada ya kufunga bao dhidi ya Ethiopia.Picha: Sunday Alamba/AP/picture alliance

Lakini beki Burkina Faso Tapsoba anafikiri klabu hiyo itafanikiwa bila ya wachezaji wao wa Kiafrika.

"Kwangu mimi kama mwanasoka kutoka Afrika, Kombe la Afrika ni mashindano maalum," Tapsoba aliiambia DW.

"Na ingawa tunaondoka Januari, tunawaamini wenzetu. Kila mtu anafanya kazi kwa bidii, na unaona kwamba kocha anajaribu kuchanganya safu katika kila mchezo. Kila mtu yuko tayari kuchukua nafasi yake, kwa hivyo tuko. Hatuna wasiwasi."

Burkina Faso walipoteza fainali yao pekee dhidi ya Nigeria, mwaka wa 2013, kwa kufungwa bao 1-0. Kwa hivyo, kushinda AFCON ni matarajio makubwa kwa Tapsoba.

"Kwa kizazi chetu, ni changamoto kwa sababu kimejaa vipaji vya vijana. Tunajaribu kufanya vizuri zaidi kuliko watangulizi wetu. Tunaenda Ivory Coast kufanya vizuri zaidi kuliko mara ya mwisho," alisema.

"Sio wakati bora "

Kikosi cha Bayer LeverkusenPicha: Revierfoto/IMAGO

Mataji mawili yanaonyeshwa kwa fahari kwenye ukumbi wa BayArena: taji la Ligi ya Ulaya lililonyakuliwa mwaka wa 1988 chini ya jina la zamani la mashindano hayo la Kombe la UEFA, na Kombe la Ujerumani (DFB Pokal) waliloshinda 1993. Leverkusen wamekaa miaka 30 bila taji.

Msururu mbaya wa klabu hiyo wa kumaliza nafasi ya pili msimu wa 2001/02 - katika Ligi ya Mabingwa, Bundesliga na Kombe la Ujerumani - uliipatia klabu hiyo jina la utani "Neverkusen".

Mkurugenzi Mtendaji wa Klabu Fernando Carro, ambaye anatamani taji, aliambia vyombo vya habari vya Ujerumani "haikubaliki" kwamba AFCON inafanyika Januari.

Lakini mkurugenzi wa michezo Simon Rolfes anatumai kuwa wataweza kukabiliana na hali hiyo.

"Jambo la Kombe la Afrika kwa hakika si bora, lakini tungependa kuwa na Kombe la Afrika katika majira ya joto ya Uropa, wakati wa mapumziko ya majira ya joto katikati ya misimu," Rolfes aliiambia DW.

"Najua kwamba wachezaji wanajivunia kuichezea nchi yao; najua tangu wakati wangu wa kucheza, ilikuwa sawa. Na tunafurahi na kujivunia kuwa tuna wachezaji wengi wa timu ya taifa wanaowakilisha nchi zao.

"Tunapaswa kukabiliana na hili. Tuna kikosi kizuri sana, na nadhani tunaweza kukabiliana na hali hii, lakini sio bora. Katika maisha, kuna baadhi ya hali ambapo unapaswa kupambana na hilo tutafanya."

Muelekeo wa kuajiri wachezaji wa Kiafrika?

Shabiki wa Senegal akishangilia kabla ya Kombe la Mataifa ya Afrika (CAN) 2021Picha: KENZO TRIBOUILLARD/AFP

AFCON inaweza kusababisha mabadiliko ambapo vilabu vikuu vya Bundesliga vinatazamia kuajiri wachezaji katika siku zijazo. Mabingwa Bayern Munich wana wachezaji watatu wa Kiafrika, ingawa ni beki wa Morocco Noussair Mazraoui pekee ndiye anayeelekea kucheza AFCON.

VFB Stuttgart itawakosa washambuliaji muhimu Serhou Guirassykwenda Guinea na Silas Katompa Mvumpa kwenda DR Congo kwa gharambe hizo.

Lakini Leverkusen itaathirika zaidi. Rolfes alisikitishwa na ukweli kwamba kuhamisha AFCON hadi msimu wa joto wa Ulaya kama ilivyotokea mnamo 2019 huko Misri hairudiwi.

"Huwezi kuwa na wachezaji 15 wa Kiafrika kwenye kikosi chako, halafu ikifika Januari, hunao tena," alisema.

 

https://p.dw.com/p/4ZjRd

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW