1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

AfD kuamua wagombea wake katika bunge la Ulaya

Angela Mdungu
29 Julai 2023

Chama cha siasa kali za mrengo wa kulia cha nchini Ujerumani AfD kinaendelea na mkutano wake wa mwaka ambapo leo Jumamosi, kitaamua majina ya wagombea katika uchaguzi ujao kwenye bunge la Ulaya.

Deutschland, Hessen, Melsungen | Das Logo der Afd ist auf die Wand projiziert beim Landesparteitag der AfD in Hessen
Picha: picture alliance/dpa

Takribani wagombea 150 wanawania nafasi kadhaa katika mchakato wa uteuzi utakaodumu kwa siku kadhaa. Moja kati ya wania nafasi hizo aliyejadiliwa jana Ijumaa ni wanachama wanaoweza kugombea ni René Aust wa jimbo la Thuringia.

Tawi la chama cha AfD la jimbo hilo lina linatajwa na shirika la kiitelijensia la mambo ya ndani ya Ujerumani kuwa lenye msimamo mkali na kwa sasa linafuatiliwa kwa karibu.

Tofauti na mpango wa awali katika mkutano huo, wagombea watachaguliwa kwanza na baadaye takribani wajumbe 600 watafanya mjadala kuhusu programu ya chama hicho kwa ajili ya kampeni za uchaguzi wa bunge la Ulaya. Hili huenda likachukua muda kufanyika hadi mwezi Januari.

Soma zaidi: Chama cha Ujerumani AfD kujiimarisha siasa za Ulaya

Hayo yanajiri wakati jana Ijumaa, chama chicho Chama kinachofuata siasa kali za mrengo wa kulia cha Mbadala kwa Ujerumani, AfD katika komngamano la mwaka kilikubali kujiunga na chama chenye itikadi kama zake cha European Identity (ID) katika ngazi ya Ulaya.

Akizungumzia hatua hiyo mwanachama wa cha AfD aliyewahi kuwa mbunge katika bunge la Ujerumani Roland Hartwig, amesema kujiunga na chama cha ID ni mbinu mpya ya kupambana na mitizamo na ukosefu wa uwajibikaji ndani ya Umoja wa Ulaya kwa chama hicho kushirikiana na washirika kutoka mataifa mengine. Ameyasema hayo baada ya kuutuhumu umoja huo kuwa umeshindwa, sio wa kidemokrasia na usioweza kufanya mabadiliko.

Mwenyekiti mwenza wa chama cha AfD Alice Weidel katika mkutano MagdeburgPicha: AFP

Chama cha European Identity ambacho AfD imetangaza kukubali kujiunga nacho ni kundi katika bunge la Ulaya linalojumuisha muungano wa vyama vya kizalendo vinavyofuata siasa kali za mrengo wa kulia kwenye Umoja wa Ulaya. Vinajumuisha chama cha kiongozi wa chama cha National Rally Party cha Ufaransa, (FPÖ) cha Marie Le Pen.

Hartwig aliwahakikishia wanachama wa AfD kuwa chama hicho kitasalia kuwa chama huru kinachojitawala ch uUjerumani hata kama kikijiunga na chama cha ID. Hata hivyo amesisitiza kuwa mkakati wa chama cha European Identity unashabihiana na ule wa AfD na kwamba chama hicho wanachojiunga nacho kinatoa kipaumbele kwa uhuru wa kitaifa.

Upinzani ndani ya AfD

Baadhi ya wanachama wa AfD wamepinga hatua hiyo ya kujiunga na chama cha ID wakisema kuwa kwa sauti yao ndani ya taifa lao wanapaza sauti kwa maslahi ya Ujerumani hata katika ngazi ya Umoja wa Ulaya, ambapo nafasi yao inabeba uzito mkubwa  na wanayo nafasi kubwa zaidi ya kufanikiwa kuliko ndani ya chama katika Umoja wa Ulaya.

Katika hatua nyingine mbunge wa chama cha  mrengo wa wastani wa kushoto cha Ujerumani SPD Fabian Funke amesema ongezeko la kura za maoni kwa chama Mbadala cha Ujerumani AfD linaleta wasiwasi.

Soma zaidi:  Scholz asema umaarufu wa AfD ni "moto wa mabua"

Hata hivyo ameiliambia shirika la habari la DW kuwa, mtihani mkubwa utakuwa katika kipindi cha uchaguzi. Funke amesisitiza umuhimu wa vyama vya kidemokrasia kufanya kazi pamoja kukabiliana na ongezeko la vyama vinavyofuata siasa kali za mrengo wa kulia.

Takwimu za hivi karibuni zilizofanywa nchini Ujerumani zinaonesha kuwachama cha AfD kilipata asilimia 20 ya uungwaji mkono na wapiga kura kote nchini humo, huku katika baadhi ya maeneo kikifikisha hadi asilimia 30 ya uungwaji mkono.