1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

AfD na matumaini ya kushinda uchaguzi wa Brandenburg

Sylvia Mwehozi
22 Septemba 2024

Chama cha siasa kali za mrengo wa kulia cha Ujerumani AfD kina matumaini ya kushinda kinyang'anyiro kikali dhidi ya chama cha Social Democrats cha Kansela Olaf Scholz katika uchaguzi wa jimbo la Brandenburg.

Uchaguzi wa Brandenburg
Boksi la kura BrandenburgPicha: Patrick Pleul/dpa/picture alliance

Chama cha siasa kali za mrengo wa kulia cha Ujerumani AfD kina matumaini ya kushinda kinyang'anyiro kikali dhidi ya chama cha Social Democrats cha Kansela Olaf Scholz katika uchaguzi wa jimbo la Brandenburg.

Chama hicho mbadala kwa Ujerumani kinachopinga wahamiaji, kwa muda mrefu kimeikosoa serikali ya muungano ya Kansela Scholz ambayo inakabiliwa na uchaguzi wa kitaifa ndani ya mwaka mmoja.

Katika uchaguzi wa leo wa jimbo la Brandenburg, AfD inalenga kupata mafanikio makubwa kama yale yaliyopatikana wiki tatu zilizopita, kiliposhinda uchaguzi wa jimbo la Thuringia na kushika nafasi ya pili katika jimbo jingine la Saxony.

Ushindi katika mji wa Brandenburg, unaozunguka mji mkuu Berlin, utazidisha shinikizo kwa chama cha mrengo wa kushoto cha SPD ambacho kimetawala jimbo hilo tangu mwaka 1990.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW